A Police officer with a gun. PHOTO/PRESS POINT

Ripoti ya William Koome

Mwanafunzi aliyemshambulia mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Ainamoi iliyoko kaunti ya Kericho amejisalimisha kwa polisi baada ya kujificha kwa takriban wiki moja.

Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu alimpiga Bw Geoffrey Rono kwa ubao uliokuwa na misumari baada ya kutakiwa kulipa baki la Sh7000 la karo.

Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 16, alijisalimisha katika kituo cha polisi cha Kapsoit.

Mwalimu mkuu huyo alitibiwa majeraha katika hospitali ya Rufaa ya Kericho kufuatia tukio hilo la Jumatano, wiki jana.